MANARA AUWASHA TENA MOTO KWA WAKONGO, ATOA LAANA KUPIGWA KWA MWANDISHI CHAMPIONI



Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amekemea tukio la AS Vita kumpiga Mwandishi wa Habari kutoka gazeti la Championi, Ibrahim Mussa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika haya yafuatayo.

Hiki kitendo wa watu wa Vita kumpiga huyu kijana anayeonekana Mwandishi wa Habari siyo cha kiungwana na kinapaswa kilaaniwe!

Kwanini hawa watu wamepaniki kiwango hiki?

Sawa, nawasihi Wanasimba msirudishie ugomvi ili wasipate sababu ya kulalamika.

Twendeni tukamalizane nao kwenye Uwanja pale Taifa usiku wa leo.

Hawa ni jirani zetu ila washapagawa na wanajua hawatoki leo, tukutane kwa Mzee Mkapa 

Dor or Die

Na Haji S Manara

Comments

Popular Posts