Skip to main content

Mbunge Msukuma aiomba serikali iupe hadhi ya Jiji mkoa wa Geita, Waziri Mkuu amjibu ombi lake (+video)



Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku almaarufu kama Msukuma leo Jumapili Machi 17, 2019 amemuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuifikiria Manispaa ya Geita kupewa hadhi ya Jiji kutokana na kukusanya mapato mengi kuliko makadirio.



Musukuma ameyasema hayo wakati akihutubia kwenye sherehe za ufunguzi wa soko la kimataifa la madini mkoani Geita, ambapo Waziri Mkuu alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi huo.
Hata hivyo, ombi lake lilijibiwa hapo hapo na Waziri Mkuu ambapo amesema kuwa kwa sasa serikali inajukumu la kuongeza miundombinu ya mikoa na wilaya mpya ila ikishakamilisha zoezi hilo basi Geita itakuwa ya kwanza kufikiriwa na kuwaasa viongozi waendelee na mikakati ya jiji.

Related Ar

Comments

Popular Posts