Paul Scholes amejiuzulu ukocha kwa meseji
Kwa mujibu wa mmiliki wa club ya Oldham Mr Abdallah Lemsagam kuwa aliyekuwa kocha mkuu wa club hiyo Paul Scholes alitangaza kujiuzulu nafasi yake ya ukocha kupitia ujumbe mfupi wa meseji, Scholes ametangaza kujiuzulu nafasi ya ukocha wa timu hiyo baada ya kudumu nayo kwa siku 31 pekee.
Sababu kubwa iliyompelekea Scholes kujiuzulu nafasi yake hiyo ni kutokana na tuhuma za kuingiliwa majukumu na mmiliki wa club hiyo, kitu ambacho hakukipenda na kuamua kubwaga manyanga akiwa ana siku 31 tu katika nafasi ya ukocha wa Oldham inayoshiriki League Two nchini England.
Pamoja na hayo Abdallah Lemsagam ambaye ndio mmiliki wa timu amekataa kuwa hakuwa ana muingilia Paul Scholes majukumu yake, Scholes amemtuhumu mmiliki huyo alikuwa anamshinikiza katika upangaji wa kikosi cha kucheza akiwa na Oldham.
Comments
Post a Comment