PSG imempiga faini ya Tsh milioni 478 Kyliane Mbappe



Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea club ya Paris Saint Germain ya nchini kwao Ufaransa Kyliane Mbappe amepigwa faini na uongozi wa club yake kufuatia kitendo chake cha uchelewaji wakati wa kikao cha timu hiyo.
Uongozi wa PSG umeamua kumpiga faini ya euro 180000 Kyliane Mbappe kama sehemu ya kumuadhibu na kumpa onyo kufuatia kitendo chake che uchelewaji katika kikao cha timu October 2018, hata sio Mbappe pekee wa PSG aliyekumbana na adhabu ya faini ni pamoja na Adrien Rabiot.
Mbappe alisaini document maalum ya kukiri kutenda kosa hilo, ambapo kiasi hicho cha euro 180000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 478 zitaenda kuchangia katika Foundation ya PSG, hata hivyo staa huyo kapewa onyo kuwa na nidhamu kwani anafuatiliwa kwa karibu na club ya Real Madrid.

Comments

Popular Posts