Taifa Stars washauriwa watumie mbinu za Simba SC kuwaangamiza Uganda

Mchezaji wa zamani wa Simba, Zamoyoni Mogella almaarufu Golden Boy ameishauri timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars kutumia mbinu ya Simba kwenye mchezo dhidi ya Uganda, The Cranes kupata ushindi.
Taifa Stars

Mchezo huo wa kuwania kushiriki fainali za Kombe la Mataifa Afrika zilizopangwa kufanyika Misri Juni mwaka huu, unatarajiwa kuchezwa mwishoni mwa wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Nyota huyo aliyetumikia timu za Simba na Stars mwanzoni mwa miaka ya 1980 hadi 1990, alisema wachezaji wa timu hiyo watumie mfano wa Simba kucheza kwa kujituma na kujitoa kurudisha fadhila kwa watanzania ambao wapo nyuma yao.

Wachukue mbinu za Simba kutumia fursa ya kuwa nyumbani kucheza kwa kujitoa wakiamini mamilioni ya Watanzania wanawategemea kuwafikisha fainali za Mataifa ya Afrika nchini Misri,‘ amesema Mogella.

Mongella amesema kuwa mchezaji unapoitwa kwenye timu ya Taifa, lazima ujisikie fahari hivyo wachezaji wanapaswa kujitoa kupigania nchi kwenye nafasi kama hiyo muhimu.

Wanatakiwa kupambana kwa dakika zote kupata pointi tatu kama tulivyofanya miaka 39 iliyopita sio kubaki kuhadithia kizazi cha sasa watu wanapenda soka,’amesema Mongella.

Taifa Stars inatakiwa kushinda huku ikiomba Lesotho ambayo ina pointi tano sawa na Stars ipoteze mchezo wake wa mwisho dhidi ya Cape Verde.
Mara ya mwisho Tanzania kufuzu fainali za michuano hiyo ilikuwa mwaka 1980 Lagos, Nigeria.

Comments

Popular Posts