AZAM FC WAPANIA KULIPA KISASI KWA MTIBWA SUGAR
OFISA Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa wapo wameanza kujipanga kwa ajili ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa uwanja wa Chamazi Mei 22 saa 2:00 usiku.
Akizungumza na Saleh Jembe, Maganga amesema wanakumbukumbu nzuri ya kupoteza mchezo wao wa kwanza msimu huu mbele ya Mtibwa Sugar kwa kufungwa mabao 2-0 hivyo hilo bado hawajasahau.
"Tuna kumbukumbu nzuri ya kufungwa mchezo wetu wa kwanza uliochezwa uwanja wa Manungu mkoani Morogoro hivyo kwa sasa tumeanza kujipanga kwa ajili ya mchezo wetu ujao.
"Mtibwa ni timu nzuri nasi tunaitambua hivyo benchi la ufundi linafanyia kazi makosa ambayo tuliyafanya kuona namna gani tutabeba pointi tatu nyumbani," amesema Maganga.
Comments
Post a Comment