HIKI HAPA KILICHOIPONZA KAGERA SUGAR KUCHAPWA MABAO 3-1 KAITABA



UONGOZI wa Kagera Sugar umesema kuwa kupoteza kwao mchezo wao wa jana mbele ya Stand United kwa kufungwa mabao 3-1 uwanja wa Kaitaba ni uzembe wa safu ya ushambuliaji kwa kushindwa kumalizia nafasi walizotengeneza.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa ni matokeo mabaya kwake kwani alikuwa nyumbani na aliamini angepata pointi tatu.

"Nilikuwa nyumbani nilijipanga kubeba pointi tatu ila haikuwa bahati yangu kwani wachezaji walishindwa kutumia nafasi ambazo walitengeneza kwenye mchezo wetu.

"Umakini na uzembe umetuponza na tumepoteza mchezo wetu, ila bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwa kuwa bado tuna michezo mkononi hivyo makosa ambayo yametokea tutayafanyia kazi," amesema.

Kagera Sugar ipo nafasi ya 15 imecheza jumla ya michezo 36 na imebakiwa na michezo miwili, kibindoni ina pointi 43.

Comments

Popular Posts