LIPULI YASHIKILIA MKATABA WA MATOLA



KOCHA wa Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa kwa sasa bado hajajua hatma yake ndani ya kikosi hicho kwani kwa sasa mkataba wake unakwenda kukamilika ndani ya kikosi hicho hivyo hatma yake wanajua viongozi wa Lipuli.

Matola ambaye ameifikisha timu hiyo hatua ya fainali ya kombe la Shirikisho msimu huu amesema anasubiri maamuzi ya uongozi juu ya hata yake.

"Mkataba wangu unakaaribia kuisha hivyo nasubiri kuona ni namna gani wanaweza kuniongezea ama nitakuwa huru kutafuta maisha sehemu nyingine," amesema Matola.

Katibu wa Lipuli, Deo Julius amesema kuwa wanatmbua kwamba mkataba wa kocha huyo unafika ukingoni hivyo watajadili hatma yake.

"Tunajua kwamba msimu unapokamilika na mkataba wa Matola unakamilika hivyo tutakaa chini kujadili hatma yake," amesema.

Comments

Popular Posts