MBALI NA KUTWAA UBINGWA, REKODI YA GENK YA MBWANA SAMATTA NI NOMA


TIMU ya KRC Genk ambayo nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta anakipiga huko jana imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Ubelgiji ikiwa ni mara ya nne.

KRC Genk imewapiku wapinzani wake wa karibu, Club Brugge ambao walipoteza mchezo wao kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Standard Liege.

Bao la KRC Genk lilifungwa na Bryan Heynen dakika ya 11 na bao la wapinzani wao lilifungwa na Yannick Bolasie dakika ya 65.


Kwenye michezo yake, Genk imekuwa na matokeo mazuri kuliko timu ya Club Brugge kwa muda wa misimu minne baada ya miaka ya 1999, 2002 na 2011.
Mchezo mmoja ambao wamebikiwa nao kwa sasa Genk ni dhidi ya Standard Liege na watakuwa nyumbani.

Comments

Popular Posts