HAJI MANARA AELEZA NYONGO YAKE YA WIVU ILE ISHU YA YANGA KUPEWA UWANJA NA MAKONDA
Imebainika kuwa Simba walikuwa wanawaonea wivu Yanga baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Jumamosi iliyopita kutangaza kuipa Yanga uwanja maeneo ya Kigamboni jijini Dar.
Makonda alitoa ahadi hiyo katika hafla ya Kubwa Kuliko ambapo Yanga iliendesha harambee ya kuichangia klabu yao.
Wivu huo wa Simba umebainika jana Alhamisi baada ya Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kumuomba Makonda na wao awapatie uwanja kama alivyofanya kwa Yanga.
Manara aliyasema hayo jana wakati akitoa neno la shukrani kwenye hafla ya kuichangia Taifa Stars iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, Dar.
Manara alisema kutokana na Simba kufanya vizuri msimu uliopita ikiwemo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kufika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika basi na wao wafikiriwe katika kupongezwa.
“Hata sisi tuna nyongo na wivu, wenzetu kule umewapa ekari saba, sisi tunakuomba hata tatu, hivi kweli timu imefika hadi robo fainali unatuacha hivihivi,” alisema Manara.
Comments
Post a Comment