HAKIKA SIMBA WAMEAMUA, SABA WA KIGENI KUPIGWA CHINI NA WAPYA KUSAJILIWA



Klabu ya Simba imepanga kuwatema wachezaji saba wa kigeni ndani ya klabu hiyo, imeelezwa.

Wachezaji wanaotajwa ni kiungo Haruna Niyonzima, James Kotea raia wa Ghana, Juuko Murshid na Emmanuel Okwi wa Uganda.

Ikumbukwe kuwa wachezaji hao wote mikataba na klabu ya Simba imeisha hivyo wako huru kwenda popote pale kuanzia sasa.

Taarifa imeeleza wengine ambao panga la Aussems linawapitia ni Nicholas Gyan raia wa Ghana, mabeki ni Asante Kwasi ambaye mkataba wake na klabu ya Simba utaisha December 2019 pamoja na Zana Coulibaly ambao mikataba yao inavunjwa ndani ya klabu hiyo.

Inasemekana wachezaji pekee wenye uhakika wa kubaki ni Mshambuliaji Meddie Kagere, Kiungo Clatous Chama na Beki Pascal Wawa.

Comments

Popular Posts