HII KALI!! KINDOKI ATAKA MILIONI 45 YANGA, SABABU ATAJA
Kumekuwa na taarifa ambazo zinaeleza kuwa klabu ya Yanga huenda ikaachana na kipa wako Mkongomani Klaus Kindoki.
Taarifa hizi zimesababisha mwenyewe kuibuka na kudai kiasi cha shilingi milioni 45 za kitanzania ili aweze kuondoka.
Imeelezwa kuwa Kindoki anataka fedha hizo ili avunje mkataba na kama asipopewa hawezi kuondoka kwa namna yoyote ile.
Licha ya tetesi za kuachwa na Yanga, awali ilielezwa kuwa Kocha wake Mwinyi Zahera alisema kuwa mabosi wake hawapaswi kabisa kumuacha.
Ilielezwa kuwa Zahera alisema Kindoki asiachwe kwani atakuwa sehemu ya msaada mkubwa ndani ya Yanga kwa msimu ujao.
Comments
Post a Comment