MABOSI YANGA WATOA TAMKO LINGINE ZITO KWA AJIBU, SIMBA YATAJWA



Licha ya Yanga kukata tamaa juu ya kumbakiza kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajibu, mabosi wa timu hiyo wamempa siku saba kwa ajili ya kuamua hatma yake kabla ya kufungwa usajili wa Shirikisho la Soka la Afrika (Caf).

Hivi karibuni Yanga waliweka hadharani kwamba licha ya kufanya jitihada za kuzungumza na kiungo huyo lakini mazungumzo yao kushindwa kufikia muafaka.

Ajibu amemaliza mkataba wake wa miaka miwili na Yanga na inatajwa kuwa kiungo huyo yupo mbioni kujiunga na Simba kwa msimu ujao.

Makamu mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema kuwa wanampa Ajibu siku hizo saba hadi Juni 30, kwa ajili ya kusikilizia maamuzi yake kabla ya kutuma majina yao ya usajili kwa Shirikisho la Soka la Afrika (Caf).

“Tunatoa siku saba tukisikilizia juu ya maamuzi ya Ajibu kama anaendelea na sisi ama la kabla hatujatuma ya usajili kufika tamati.

“Si busara sisi tumeona Yanga kukaa tu tukimng’ang’ania wakati ambao mkataba wake unaisha tukaja kumkosesha kucheza michuano ya kimataifa, bora aamue mapema ili tujue tunafanya nini,” alisema Mwakalebela.

Mkataba wa Ajibu na Yanga unagota ukingoni Juni 30, mwaka huu.

Comments

Popular Posts